Aliyekuwa mkuu wa DCI Kinoti alihamia Tume ya Utumishi wa Umma

Hii inafuatia "kujiuzulu" kwake kama alivyotangaza Ruto, baada ya kutumikia nchi kwa miaka 30.

Muhtasari
  • Tume hiyo inatafuta kuajiri DCI mpya na mahojiano yataanza wiki ijayo
  • PSC sasa itampeleka kwenye wadhifa wowote serikalini
DCI George Kinoti
DCI George Kinoti
Image: MAKTABA

Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi Alhamisi iliidhinisha uhamisho wa huduma za aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai George Kinoti hadi Tume ya Utumishi wa Umma.

Hii ni kwa masharti kwamba Kinoti atasalia na malipo na marupurupu ya kibinafsi kwake, kuanzia Septemba 27 2022 hadi kufikia umri wa lazima wa kustaafu.

Hii inamaanisha kuwa Kinoti alijiuzulu kama mkurugenzi wa DCI lakini akabaki afisa katika Huduma ya Kitaifa ya Polisi.

PSC sasa itampeleka kwenye wadhifa wowote serikalini.

Kinoti aliondoka DCI mnamo Septemba 30, 2022, baada ya kuhudumu kwa miaka minne ya muhula wake wa miaka sita.

Kinoti, DCI wa 11 alikabidhi ofisi kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu mpya Dkt Hamisi Masa.

Hii inafuatia "kujiuzulu" kwake kama alivyotangaza Ruto, baada ya kutumikia nchi kwa miaka 30.

DCI aliyemaliza muda wake alijiunga na Polisi wa Kenya mwaka wa 1992 kama afisa wa kuajiri na akapanda vyeo na kuwa afisa mkuu wa upelelezi nchini.

Tume hiyo inatafuta kuajiri DCI mpya na mahojiano yataanza wiki ijayo.