(+PICHA)Raila awasili katika uwanja wa Kamkunji kuongoza mkutano

Anatarajiwa kufichua maelezo ya madai ya "jinsi ushindi wake wa urais ulivyoibiwa".

Muhtasari
  • Baada ya kuwasili kutoka Afrika Kusini, msafara wa Raila ulitumia Barabara ya Mombasa kuelekea Haile Selassie alipokuwa akielekea Kamukunji
KINARA WA AZIMIO RAILA ODINGA BAADA YA KUWASILI KATIKA UWANJA WA KAMUKUNJI 23/01/2023
Image: ANDREW KASUKU

Kiongozi wa ODM Raila Odinga aliwasili katika uwanja wa Kamkunji kwa mkutano wake mkubwa mwendo wa saa nane unusu alasiri.

Anatarajiwa kufichua maelezo ya madai ya "jinsi ushindi wake wa urais ulivyoibiwa".

Baada ya kuwasili kutoka Afrika Kusini, msafara wa Raila ulitumia Barabara ya Mombasa kuelekea Haile Selassie alipokuwa akielekea Kamukunji.

Umati ulionekana kumpokea alipokuwa akiwapungia mkono Wakenya katika soko la Gikomba, huku wengine wakikusanyika katika uwanja wa Kamukunji kabla ya kuwasili.

(Kushoto)KINARA WA WIPER KALONZO MUSYOKA,RAILA ODINGA NA MARTHA KARUA KATIKA UWANJA WA KAMUKUNJI 23/01/2023
Image: ANDREW KASUKU

Raila anaandamana na Martha Karua (Narc Kenya), Kalonzo Musyoka (Wiper), Eugene Wamalwa (DP), na George Wajackoyah (Chama cha Roots) miongoni mwa viongozi wengine waliochaguliwa.

RAILA ODINGA NA MARTHA KARUA
Image: ANDREW KASUKU
 

Mkuu huyo wa upinzani amekuwa nchini Afrika Kusini kwa ziara ya wiki moja katika wadhifa wake kama Mjumbe Maalum wa Umoja wa Afrika kuhusu Miundombinu.

KINARA WA AZIMIO RAILA ODINGA
Image: ANDREW KASUKU
KINARA WA AZIMIO RAILA ODINGA
Image: ANDREW KASUKU