Msuada wa fedha utatipitshwa vile ilivyo - Cherargei

Alimshtumu Raila kwa kukaa kimya wakati utawala uliopita ulikua ukikukopa.

Muhtasari

• Kulingana na seneta huyo wa UDA, Bunge halitakuwa na budi ila kupitisha Mswada huo bila mabadiliko yoyote.

• Aliendelea kusema kuwa serikali ilikua na mawili ya kuchagua, kukopa au kuongeza mapato kwa njia ya kodi.

Seneta wa Nandi Samson Cherargei.
Seneta wa Nandi Samson Cherargei.
Image: STAR

Seneta wa Nandi Samson Cherargei sasa anasema kuwa mswada wa Fedha 2023 unaopendekezwa na serikali ya UDA hautabadilishwa hata koma.

Kulingana na seneta huyo wa UDA, Bunge halitakuwa na budi ila kupitisha Mswada huo bila kufanya mabadiliko yoyote bila kuongeza ama kupunguza koma.

Aliendelea kusema kuwa serikali ina njia mbili pekee kukidhi bajeti yake, kukopa au kuongeza mapato kwa njia ya kodi.

Cherargei alisema Wakenya sasa wanalipa deni la trillioni 10 ambalo lilitokana na serikali ya awali iliyoongozwa na Uhuru Kenyatta.

"Kwenye Mswada wa Fedha wa 2023, uamuzi wa kupitishwa na Bunge sio wa hiari ambapo hata koma haitarekebishwa kwa sababu tunakopa zaidi au kuongeza mapato yetu kwa njia ya ushuru. Deni kubwa la Sh10 trilioni liliwekwa na serikali ya handsheki ya Uhuru na Raila ambalo Wakenya wanalipa sasa," seneta huyo wa Nandi alisema.

Aidha amemkashifu kinara wa Upinzani Raila Odinga kwa kukaa kimya wakati serikali ya awali iliendelea kukopa.

"Raila hakuleta pingamizi yoyote katika serikali ya handisheki licha ya kuwa mshauri mkuu wa Uhuru basi unapaswa kukomesha unafiki huu. Hii ni kwa sababu hakuna ushuru mpya unaoletwa nchini. Kulipa ushuru ni kujitegemea!" Cherargei aliongeza.

Kiongozi wa Azimio Jumatatu aliziita mapendekezo ya sheria ya ushuru ya Rais William Ruto kama "kipande cha adhabu".

Muswada huo, pamoja na mambo mengine, unapendekeza kuongezwa kwa mchango ya bima ya hospitali (NHIF), hasa kwa watu wenye kipato kikubwa.

Pia msuada hio inapendekeza makato ya lazima ya asilimia tatu ya mshahara kwa hazina ya nyumba na kuongeza ushuru kutoka asilimia 30 ya sasa hadi asilimia 35 kwa wale wanaopata Sh500,000 na zaidi.