Tumepunguza sumu-Ujumbe wa Sifuna baada ya Serikali kupunguza ushuru wa nyumba kutoka 3% hadi 1.5%

Haya yanajiri huku mswada wa fedha ukitarajiwa kwasilishwa bungeni siku ya Jumanne.

Muhtasari
  • Kupunguzwa kwa ushuru wa nyumba unajiri siku chache baada ya mcheshi Eric Omondi kusema kwamba mpango huo wa nyumba sio wa dharura.
b6251efb2cdb00bc
b6251efb2cdb00bc

Katibu Mkuu wa chama cha Orange democratic movement ODM Mhe Edwin Sifuna ambaye pia ni Seneta wa Nairobi amejibu kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter saa chache baada ya serikali ya Kenya Kwanza kupunguza ushuru wa nyumba kutoka 3% hadi 1.5%.

Kulingana naye Wakenya wanapaswa kukataa Mswada mpya wa Fedha wa 2023 unaopendekezwa iwapo rais William Ruto aupunguze.

Baada ya kusikiliza kwa makini maoni yaliyotokana na mazungumzo makali kuhusu hali ya nyumba na hazina ya nyumba, Rais William Ruto amechukua mapendekezo ya kupunguza ushuru wa nyumba kutoka 3% hadi 1.5%. 

“Tumepunguza sumu, sasa kuleni,"Alisema Seneta Edwin Sifuna.

Kupunguzwa kwa ushuru wa nyumba unajiri siku chache baada ya mcheshi Eric Omondi kusema kwamba mpango huo wa nyumba sio wa dharura.

“ Nafikiri mazungumzo haya yanayohusu ujenzi wa nyumba kwa sasa ni makosa kuyazungumzia. Serikali ya Kenya Kwanza ilituahidi maisha mazuri na rahisi watakapofuzu katika uchaguzi. Rais mwenyewe alizungumzia kumhusu mama mboga na mtu wa bodaboda, mimi binafsi nimekatwa mara nne, nimekutana na watu wa bodaboda huko ambao wamekamatwa kwa makosa madogo sana.”

Omondi aliendelea kusisitiza kuwa hakuna mtu asiye na makao. Alieleza kwamba Juni 1 wakati taifa lilikuwa likisherekea maadhimisho ya siku ya madaraka ya miaka 60 raia wamekuwa na kwa kuishi kwa miaka yote hiyo.

“Hakuna mtu ambaye hana kwa kuishi, hata mjomba wangu mwenyewe anayeishi katika vibanda vya Kibera, anachohitaji sasa hivi ni chakula na maji.Kuna baadhi ya vitu binadamu hawezi kuishi bila; chakula, maji, na afya.”

Haya yanajiri huku mswada wa fedha ukitarajiwa kwasilishwa bungeni siku ya Jumanne.