Oscar Sudi ameapa kutochukua hatua dhidi ya wakenya waliopora klabu yake

Sudi alisikitishwa kwamba wahuni waliwapiku Gen Z kwenye maandamano na kulenga biashara yake.

Muhtasari

•Klabu ya mbunge Oscar Sudi,Timba XO  iliharibiwa na waporaji, huku bidhaa za kifahari zikiporwa.
•Hata hivyo mbunge huyo alidai kuwa hana ulinzi wowote wa kulinda mali  yake.

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi
Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi
Image: MAKTABA

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ameapa kutochukua hatua dhidi ya raia waliopora nakuchukua bidhaa kwa klabu yake inayojulikana kama Timba XO.

Klabu hio inayopatikana Eldoret karibu na barabara ya Eldoret kuelekea Nairobi iliporwa na baadhi ya watu wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha mjini Eldoret.Huku wengi wakitoroka na bidhaa za kifahari.

Oscar Sudi alitoa taarifa kupitia video ambayo imeenea kwenye mitandao ya kijamii huku akidai kuwa yeye hajawahi kosea popote

"Nataka niseme maneno mawili juu ya hili pambano la 'wakalenjin' tangu nizaliwe najua kujenga, iwe darasani, shule, makanisa sijawahi kujua kuharibu kitu cha mtu, mambo niliyoyaona juzi kwenye kata wakati wanaharibu. kaunti na kuharibu biashara yetu kama vile Club Timba..."

Aidha Sudi,alielezea kuhusu maandamano yaliyotokea Jumanne 25 akitaja kuwa ni jambo la kusikitisha.

"Kilichotokea Jumanne ,baada ya maandamano ya amani ya kizazi kipya,ni jambo l kusikitisha.Hata hivyo,ukubwa wa upotevu wa maisha,uporaji na uharibifu wa mali uliotokea ni wa kutisha na unakiuka roho ya katiba yetu.Katika maisha yanguyote sijawahi kuandaa au kutakia mabaya washindani wangu wa kisiasa..."

Aidha alisema kuwa ameamua kusimamisha shughuli zake zote za siasa na kudai kuwa hana ulinzi wa kulinda mali zake.