Picha ya mwanaume amening'inia nyuma ya gari na jeneza yazua mjadala

Wengine walisema jeneza hilo ni la jamaa huyo

Muhtasari

• “Sioni chochote kibaya hapa sababu ameshakufa kwa nini asichukuliwe safari yake ya mwisho ya kutishia mzimu,” mwingine alitoa maoni.

Mwanaume alionekana amejining'iniza nyuma ya gari na jeneza
Mwanaume alionekana amejining'iniza nyuma ya gari na jeneza

Wiki hii, picha moja ya gari linalodhaniwa kuwa la uchukuzi wa umma likiwa na mwanaume aliyening’iniwa kwa nyuma pamoja na jeneza imesambazwa sana kweney mitandao ya kijamii.

Picha hiyo ilisemekana kuchukuliwa katika barabara moja nchini Zimbabwe, kutokana na nambari za usajili za gari lile inaoneza jeneza limefungwa nyuma huku mwanaume amening’inia kando yake huku akilishikilia jeneza lile ilizua gumzo kali mitandaoni huku baadhi wakikisia kwamba lilikuwa limebeba maiti na mwanaume huyo alikuwa anashikilia ili kuepusha lisidondoke.

Wengine walisema lilikuwa ndio linaenda kuchukua maiti kutoka makafani.

Kilichozua mjadala mkali ni kwa jinsi jeneza hilo lilikuwa limetingwa kwa Kamba nyingi na tukio la mwanaume huyo kujining’iniza pale pia lilizua mjadala changamano hata zaidi huku baadhi wakisema kwamab hawaoni tatizo na kitendo hicho kwani mtu tayari akishakufa hana dhamani duniani.

Wengine walimtetea mwanaume yule kwa kusema kwamba hakuna tatizo akijining’iniza ili kusaidiwa kufika alikokuwa akienda.

“Sioni chochote kibaya hapa... Abiria huyu anapaswa kupewa lifti nje. Ni yeye, au mimi ndani ... Hatuwezi kuwa sisi sote!” Mmoja kwa jina Elsie Globler aliandika.

“Sioni chochote kibaya hapa sababu ameshakufa kwa nini asichukuliwe safari yake ya mwisho ya kutishia mzimu,” mwingine alitoa maoni.

Oh my freaking word

Posted by SA Long distance Truckers on Sunday, September 4, 2022

Wengine walisaili ni kwa nini jeneza hilo halikufungwa juu ya gari hilo kwani hivyo ingekuwa afadhali zaidi kuepusha minong’ono kama hilo mitanaoni.

“Lipo tupu natumai, lakini siku hizi majeneza yanatumika kwa kila aina ya vitu sio maiti tu,” mwingine alisema.

Wengine pia walibishana kwamba huenda jeneza hilo ni la huyo jamaa na kitendo cha kujining’iniza kando yake ni ishara ya kutoa ulinzi kwa mali yake.

Maoni yako kwa hii picha ni yepi?