Sonko achukizwa na Uingereza kuwasafirisha marais wa Afrika kwenye basi moja

Hawa wazungu hawana adabu - Mike Sonko.

Muhtasari

• Ruto alionekana kweney basi pamoja na marais wengine huko Marekani wakielekea katika msiba wa malkia Elizabeth II.

Mike Sonko amechukizwa na hatau ya Uingereza kuwasafirisha marais wa Afrika kwenye baso moja
Mike Sonko amechukizwa na hatau ya Uingereza kuwasafirisha marais wa Afrika kwenye baso moja
Image: facebook

Mfanyibiashara maarufu na ambaye alikuwa gavana wa pili wa Nairobi Mike Sonko ameonyesha kuchukizwa kwake na picha inayosambazwa mitandaoni ikionesha rais William Ruto akiwasili kwenye mazishi ya malkia Elizabeth wa pili kwenye basi.

Rais Ruto aliondoka nchini Wikendi iliyopita akiandamana na mkewe kuelekea Uingereza kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya malkia Elizabeth II ambaye alifariki wiki moja iliyopita.

Hii ilikuwa ni ziara yake ya kwanza kabisa nje ya nchi kama rais. Hafla hiyo ya msiba ilisemekana kuhudhuriwa na marais kutoka mataifa takribani 200 kote duniani.

 Katika picha hiyo, rais Ruto na mama wa taifa Rachael Ruto wanaonekana wameketi ndani ya basi kuelekea katika eneo la msiba. Ni picha ambayo imeibua mjadala mkali mitandaoni huku Waaafrika wengi wakisema kwamba marais kutoka mataifa ya Afrika walitumia mabasi kuwasili eneo hilo huku marais wa mabara mengine wakifika kwa njia ya kifahari, ndege.

Sonko ni mmoja wa wale ambao wameingia kwenye mitandao ya kijamii na kutolea maoni yao kuhusu picha hiyo ambapo anahisi Wazungu wanawakosea Waafrika heshima kwa kuwasafirisha marais wao kama abiria wengine wasio na cheo.

“Hawa wazungu hawana adabu wanawekaje marais wa Africa ndani ya Bus moja huko London. Mungu tatuhurumie, kitu mbaya ifanyike kwa hiyo basi itakuaje?” Sonko aliuliza kwa ghadhabu.