Kutumia vyombo vya habari kunitisha hakutafaulu-Miguna amwambia Raila

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter siku ya Jumatatu alimtumia kinara wa ODM,Raila Odinga ujumbe.

Muhtasari
  • Katika ujumbe wake,alimtaarifu Odinga kwamba siku ya Ijumaa ataenda Kisumu,Kaunti ambayo inafahamika kuwa maeneo makuu ya kinara huyo
Jenerali Miguna hatimaye ametua nchini
Jenerali Miguna hatimaye ametua nchini
Image: Andrew Kasuku

Wakili MIguna MIguna amekuwa akigonga vichwa vya habari baada ya kurejea nchini kutoka Canada.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter siku ya Jumatatu alimtumia kinara wa ODM,Raila Odinga ujumbe.

Katika ujumbe wake,alimtaarifu Odinga kwamba siku ya Ijumaa ataenda Kisumu,Kaunti ambayo inafahamika kuwa maeneo makuu ya kinara huyo.

"@RailaOdinga : Kutumia Githeri Media KUNITISHIA haitafanya kazi. Ninakuja Kisumu siku ya Ijumaa. Endelea na ujihusishe na VURUGU na GHARAMA. Hiyo ndiyo sifa yako ya msingi. Lakini mwishowe, Taifa la Wajaluo na lazima LIKOMBOLEWE."

Kutokana na habari kuhusu madai ya Miguna kwamba Raila alimtishia kupitia vyombo vya habari na kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, mijadala mingi inazushwa kwa sasa.

Wanamitando wametoa hisia mbambali kutokana na ujumbe wa Miguna, huku baadhi yao wakimuunga mkono na wengine wakimuonya wakili huyo akome kumtaja Raila.

Miguna alirejea nchini 20/10/2022 baada ya takriban miaka 4 ya kufurushwa.