Msichana wa miaka 3 amuua dadake wa miaka 4 kwa kumfyatulia risasi

Msichana huyo wa umri wa miaka 3 alipata bastola iliyojaa na kufyatua risasi moja kwa dadake wakiwa chumbani.

Muhtasari

• Visa vya mauaji kwa kwa matumizi ya kiholela ya bunduki vimekithiri katika taifa hilo lenye wingi wa bunduki kuliko watu,

Mwanafunzi ajiua kwa kujipiga risasi Kilimanjaro
Mwanafunzi ajiua kwa kujipiga risasi Kilimanjaro
Image: YoutubeScreengrab

Msichana wa miaka 3 anashikiliwa kwa mahojiano Zaidi baada ya kumuua dada yake wa miaka 4 kwa kumfyatulia risasi kwa bunduki wakiwa nyumbani.

Kisa hicho kiliripotiwa na runinga ya CBS na katika klipu ambayo ilichapishwa kwenye wavuti wao, msichana huyo walikuwa wanaishi huko Texas na ilisemekana kwamba alimuua dadake kwa bahati mbaya.

Sherifu wa Kaunti ya Harris Ed Gonzalez alisema wasichana hao walikuwa katika chumba cha kulala cha ghorofa huko Houston, ambapo waliishi na wazazi wao, na tukio hilo lilijiri mwendo wa saa mbili usiku.

Watu wazima watano, ambao wote walikuwa wanafamilia au marafiki wa familia, walikuwa katika sehemu zingine za ghorofa na wasichana bila kukusudia waliachwa bila usimamizi, Gonzalez alisema.

Alisema mzazi mmoja alidhani mwenzie alikuwa akiwatazama wasichana hao, wakabaki peke yao chumbani. Msichana huyo wa umri wa miaka 3 alipata bastola iliyojaa na kufyatua risasi moja, sheriff alisema.

"Mtoto mwenye umri wa miaka 3 alipata bastola iliyokuwa imepakiwa na nusu-otomatiki. Wanafamilia walisikia mlio wa risasi moja. Walikimbilia chumbani na kumkuta mtoto mdogo, mwenye umri wa miaka 4, asiyeitikia," Gonzalez alisema.

Msichana huyo alitangazwa kufariki katika eneo la tukio baada ya polisi kuitikia wito wa 911 wa familia, Gonzalez aliwaambia waandishi wa habari nje ya nyumba hiyo.

"Inaonekana kama hadithi nyingine ya kusikitisha, tena, mtoto kupata bunduki na kuumiza mtu mwingine na wakati huu kulikuwa na risasi mbaya," Gonzalez alisema.