Mama afariki baada ya kushiriki mapenzi na mtoto wake wa kumzaa mwenye miaka 15

Inadaiwa mama huyo baada ya kufumaniwa katika kitendo na mtoto wake, alipelekwa kituo cha polisi lakini akafariki kwa mshtuko wa moyo.

Muhtasari

• Polisi wanamshikilia mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka 15 kwa kosa la kujamiiana na mamake mzazi.

• Mama huyo alizikwa saa chache baadae kulingana na mila za kidini.

Jeneza la Marehemu
Image: HISANI

Kisa kisicho cha kawaida kilishuhudiwa katika mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania baada ya mwanamke aliyedaiwa kushiriki mapenzi na mwanawe wa kumzaa kufariki kwa mshtuko wa moyo.

Kulingana na ripoti iliyopeperushwa na blogu ya Ayo Tv, Mama huyo aliyetamuliwa kwa jina la Clemensia alifariki dunia baada ya kukimbizwa katika Hosptali ya Rufaa ya Mawenzi akitokea kituo cha Polisi Moshi alipokuwa akishikiliwa na Polisi mkoani Kilimanjaro kwa kosa la kufanya mapenzi na mtoto wake wa kumzaa.

Wakaazi wa mkoa huo ambao walikuwa katika mapokezi ya mwili wake kwa ajili ya maziko walielezea kisa kisicho cha kawaida ambapo gari la kubeba maiti lilipotoka mochwari na kuingia barabara kuu kuelekea makaburini lilizima ghafla na kugoma kwenda.

“Vitu vilivyotokea ni kwamba gari liliingia vizuri mochwari likachukua mwili na lilipoingia katika barabara kuu likazima. Likawashwa mara kadhaa bila mafanikio,” mkaazi mmoja alisimulia.

Baadae gari hilo liliwaka baada ya mtoto wa marehemu wa kike kushuka katika gari hilo.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Saimon Maigwa alikiri kupokea taarifa za tukio hilo na kusema Jeshi la Polisi bado linamshikilia mtoto wa kiume wa mwanamke huyo mbaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 15 kwa kosa la kufanya mapenzi na mama yake mzazi ambaye kwa sasa ni Marehemu.

Haijabainika mtoto huyo atashtakiwa kwa kosa gani ikizingatiwa kwamba mtuhumiwa mwenza ambaye ni mamake tayari ameshafariki na yeye yuko chini ya umri wa miaka ya utu uzima kisheria.