HAJI KUJITETEA BUNGENI

DPP Doordin Haji ajitetea mbele ya wabunge

Pia rais ameona thamani yangu akiniteua katika idara hiyo

Muhtasari

• Nyumba yangu ilivunjwa,nilifikishwa mahakamani mara nyingi,zaidi ya kesi 20 nilishtakiwa kwazo katika kipindi cha miaka miwili.

• NIS si shirika ambapo unaweza amka siku moja na useme unaenda kumtukunu  mtu kwa sababu ya kazi nzuri ambayo amefanya.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji
DPP Norrdin Haji Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji
Image: Maktaba

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma DPP Doordin Haji amevunja kimya chake na kutoa sababu ya kuteuliwa na rais Ruto katika idara ya upelelezi,NIS. 

Haya yanajiri wakati alipokuwa akihojiwa na wanakamati kwenye kikao cha bunge kilichoandaliwa City Hall Mei 30 kuhusiana na hali ya usalama nchini.“ Nilitishiwa sana lakini sikunasika katika tisho lolote.” Haji alikiri.

Aliendelea kueleza kuwa,hadi nyumba yake ilivunjwa na kuibiwa,mara si moja kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kesi zaidi ya ishirini chini ya muda wa miaka miwili.“ Nyumba yangu ilivunjwa,nilifikishwa mahakamani mara nyingi,zaidi ya kesi 20 nilishtakiwa kwazo katika kipindi cha miaka miwili.” DPP alieleza.

Haji alieleza kuwa kazi hiyo anakusudia kuipata iwapo ataidhinishwa na wabunge, si zawadi. Alikiri kuwa idara ya NIS si shirika ambapo unaweza amka siku moja na useme unaenda kumtukunu  mtu kwa sababu ya kazi nzuri ambayo amefanya.“ NIS si shirika ambapo unaweza kuamka na useme unamzawadi mtu kwa sababu amefanya kazi nzuri. Mafikra mengi yameweza kuangaziwa, na pia rais ameona thamani yangu kama mteule wake katika idara hiyo” Aliendelea.