Akaunti ya FB ya benki kuu ya Zambia yadukuliwa, mdukuzi aweka picha watu wakibusiana

Akaunti hii inatangazwa kudukuliwa miezi michche baada ya akaunti ya Facebook ya chuo cha Kabarak kudukuliwa.

Muhtasari

• Kwa hivyo, Mwanza alituma tahadhari kwa umma kutoingiliana na ukurasa ulioathirika hadi itakapotangazwa tena.

• "Benki ya Zambia inasikitika kuwafahamisha umma kuhusu tukio la usalama wa mtandao lililoathiri ukurasa wa Facebook wa benki.”

Akaunti ya Facebook ya BOZ yadukuliwa.
Akaunti ya Facebook ya BOZ yadukuliwa.
Image: Screengrab

Wadukuzi wamechukua ukurasa wa Facebook wa Benki ya Zambia (BoZ), na kulazimisha Benki Kuu kufanya uhakiki wa kina wa matukio hayo.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu na kuchapishwa kwenye majarida ya nchini humo, Benki Kuu ilidokeza kuwa inafanya juhudi zote kuhakikisha ukurasa huo unarejeshwa.

Ilisema kupitia kwa Mkurugenzi wake Msaidizi wa Mawasiliano, Besnart Mwanza, imekutana na vyombo vya sheria kushughulikia suala hilo.

Kwa hivyo, Mwanza alituma tahadhari kwa umma kutoingiliana na ukurasa ulioathirika hadi itakapotangazwa tena.

"Benki ya Zambia inasikitika kuwafahamisha umma kuhusu tukio la usalama wa mtandao lililoathiri ukurasa wa Facebook wa benki.”

“Tunafanya uhakiki wa kina wa matukio hayo na kufanya kazi kwa karibu na wasimamizi wa sheria ili kuhakikisha kuwa yanashughulikiwa. Benki inafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa jukwaa linarejeshwa katika utendaji wake kamili haraka iwezekanavyo,” Mwanza alisema.

"Tunasikitika kwa usumbufu uliojitokeza," Mwanza aliongeza.

Wimbi la udukuzi wa akaunti za taasisi za nchi linaendelea kukumba watu wengi.

Utakumbuka miezi michache nyuma, kudukuliwa kwa akaunti ya Facebook ya chuo kikuu cha Kabarak ilidukuliwa na kijana huyo mwenye usuli wa bara la Asia aliweka picha zake na hata kuchapisha wazi wazi kwamba alikuwa anataka kulipwa kabla ya kuirudisha.

Uongozi wa chuo hicho hata hivyo haikutoa tamko lolote licha ya jamaa huyo kutamba kwa machapisho mengi ya kufurahisha na kughasi vile vile.

Baada ya takribani wiki moja, Kabarak walifanikiwa kuichukua akaunti yao katika mchakato ambao hawakuweka wazi lakini walitoa shukrani zao kwa timu yao ya kiteknolojia kufanikisha hilo.