- Lsk inamtaka rais kuvunjilia bunge kama alivyoshauri jaji Mkuu
- Havi anasema wabunge hawana tena maamlaka ya kuwaakilisha wakenya
Rais wa Chama cha mawakili nchini LSK Nelson Havi ametibitisha kwamba wamewaarifu maspika na makarani wa bunge la taifa na senate kuhusu nia yao ya kuingia majengo ya bunge hapo kesho.
Kampeini hyo kwa jina 'Occupy Parliament' ndio jitihada ya hivi punde ya LSK kumshurutisha rais Uhuru Kenyatta kulivunja bunge kama alivyoshauri jaji mkuu David Maraga .
Mwingine aliyepewa taarifa ya kwenda bungeni ni inspekta mkuu wa Polisi ambaye LSK inamtaka atoe ulinzi wa maandamano hayo ya kuingia bungeni kuanzia saa nane unusu alasiri .
Katika notisi yake LSK inasema bunge limepoteza maamlaka ya kutunga sheria kwa nia ya wakenya .
Kando na LSK makundi mengine yanayoshirikishwa katika mpango huo wa kuingia bungeni ni United Green Movement (UGM) na Weare52pc.