Wazee wanatarajia kurahisha azma ya Odinga kumrithi Raia Uhuru 2022

Je,Itatosha kwa wazee wa Kikuyu Kusema ‘Raila Tosha?’ Odinga awakaribisha kwake Bondo

Mkutano huo ni jitihada za kuziunganisha jamii za Waluo na Wakikuyu kabla ya uchaguzi mkuu ujao

Muhtasari
  •  
     Mbunge Maina Kamanda na mbunge wa zamani Peter Kenneth wapo katika ujumbe huo
  •  Kutakuwa na mkutano mwingine wa wazee wa walio kwenda Nyeri

 

Raila Odinga

 Kiongozi wa ODM Raila Odinga  siku ya jumamosi  alikuwa mwenyeji wa mamia ya wazee kutoka jamii ya Wakikuyu nyumbani kwake Bondo katika kaunti ya Siaya .

 Wazee hao na wanasiasa kadhaa kutoka ngome ya rais Uhuru Kenyatta ya Mlima Kenya  wanatarajiwa kumwidhinisha Odinga kuwa rais mwaka wa 2022 .

Raila,  alikosa kuhudhuria hafla ya mamombi ya kitaifa katika Iulu ili kuwaalika wazee hao nyumbani kwake .Mamia ya wananchi walionekana wamefurika boma hilo linalotambulika kama  Kango Kajaramogi.

 Katika picha  zilizowekwa wenye Twitter  wazee hao wamevalia  kwa njia ya kitamaduni ili kuashiria umuhimu wa safari yao .

 “Muhammad Ali  alituambia s “ Urafiki ndio kitu kigumu sana kueleza . Sio jambo unalofunzwa shuleni .lakini iwapo hujui maana ya urafiki ,hujajifunza lolote’ alindika Raila katika Twitter .

 “ Tunashuhudia alichomaanisha Ali wakati mimi na Mama Ida tunapowakaribisha viongozi kutoka Mlima Kenya’ aliongeza

 Mbunge Maina Kamanda na aliyekuwa mbunge wa Gtanga  Peter Kenneth ni miongoni mwa wanasiasa katika ujumbe wa wazee hao .

 Kakake mkubwa Raila Oburu Odinga ,gavana Cyprian Awiti na Peter Kennth ndio miongoni mwa walioketi mstari wa mbele katika jukwaa kuu .

 

 

Mama Ida Odinga na Mbunge Maina Kamanda
Wazee wa jamii ya Kikuyu katika hema,Bondo