- Hakutakuwa na ukaguzi wa walio na virusi vya corona katika maeneo ya mipakani
- Wamesema baadhi yao wamesalia katika nafasi moja kwa miaka zaidi ya 15
Huduma katika hospitali za umma huenda zitalemazwa kuanzia saa sita usiku wa kuamkia alhamisi .
Hii ni baada ya wafanyikazi wa sekta ya afya kutishia kuanza mgomo wao ili kulalamikia walichokitaja kama kufeli kwa serikali kuu kushughulikia lalama zao kuhusu kupandishwa vyeo.
Mgomo huo utavuruga utoaji wa huduma katika vituo vya afya katika viwanja vya ndege , vituo vya mipakani hospitali ya kushughulikia majeraha y auto wa mgongo
Hospitali nyingine zitakazoathiriw ana mgomo huo ni Mathari , Othaya , Benki ya kitaifa ya damu ,maabara za umma na vituo vuote vya afya vinavyohudumiwa na wafanyikazi wa wizara ya afya .
" Ni bahati mbaya sana kwamba wakati huu wa janga la corona tunawapa habari hizi mbaya .hakutakuwa na vipimo vya Covid 19 katika maeneo yote ya kuingia nchini’ amesema mwenyekiti wa muungano wa kitaifa wa maafisa wa kliniki Peterson Wachira .
" Tumelaghaiwa hapo awali mara kadhaa na hatutakubali mtido huo kwani sisi sio watoto’
Miungano mingine itakayohusika na mgomo huo ni muungano wa kitaifa wa wauguzi ,muungano wa wahudumu wa afya ,maaafisa wa maabara kote nchini ,muungano wa kitaifa wa wanafamasia na wahudumu wa sekta nyingine za afya .
Miungano hiyo imesema kwamba ni jambo la kuwaondoa motisha kwamba wizara ya afya kwa miaka mingi imeahidi kutekeleza mpango wa kuwapandisha vyeo na ngazi kazini lakini imekuwa ikitumia njia za kuchelewesha ahadi hizo .
Kwa sababu ya hatua hiyo baadhi ya wanachama wao wamekuwa katika ngazi moja ya kazi kwa Zaidi ya miaka 15