- Matamshi yake yanajiri baada ya rais Uhuru na Raila kulegeza misimamo yao kuhusu kurekebisha baadhi ya mapendekezo katika ripoti ya BBI .
- Cherargei amesema kamati mpya ya usimamizi wa mchakato wa BBI inafaa kuwa na uwezo wa kushughulikia masuala yote ynayoibuka kutoka sekta zote na matabaka ya watu
Seneta wa Nandi Samson Cherargei amemshauri rais Uhuru Kenyatta kuunda kamati nyingine mpya ya BBI ili kukusanya maoni ya wakenya .
Seneta huyo amesema kuwasilisha mapendekezo kwa kiongozi wa ODM Raila Odinga sio hakikisha kwamba marekebiusho hayo yatawekwa katika ripoti ya mwisho .
Matamshi yake yanajiri baada ya rais Uhuru na Raila kulegeza misimamo yao kuhusu kurekebisha baadhi ya mapendekezo katika ripoti ya BBI .
“ Makundi haya yametoa mapendekezo ya kuirekebisha ripoti hiyo ,wataapeleka wapi?’ Cheraragei amehoji
“ kwa maoni yetu tunamtaka rais atumie kasi kuunda kamati nyingine ya BBI ili ifanye kazi ya kukusanya mapendekezo ya wakenya . Kuwasilisha maoni hayo kwa kiongozi wa ODM sio jambo linalofaa kwa sababu hana uwezo wa kuyajumuisha yote katika ripoti ya mwisho kama inavyofaa’
Cherargei amesema kamati mpya ya usimamizi wa mchakato wa BBI inafaa kuwa na uwezo wa kushughulikia masuala yote ynayoibuka kutoka sekta zote na matabaka ya watu .
Seneta huyo amesema marekebisho ya katiba ni jambo ambalo linafaa kuwahusisha watu wote na halifai kuingizwa siasa .
“ Nimefurahi kwa sababu kuna fursa ya kutoa mapendekezo . baadhi ya viongozi hata bungei walikuwa wametuambia kwamba hakuna hata koma itakayoongezwa au kutolewa katika ripoti hiyo’
Siku ya jumatatu Raila alikutana na viongozi kutoka jamii ya wafugaji wa kuhama hama wakiongozwa na waziri wa Fedha Ukur Yatani na baadaye wakasema wataiunga mkono iwapo baadhi ya sehemu zitabadilishwa