Patanisho?

Uhuru akutana na Ruto kwa saa 3 katika mkutano ulIofanyika Ikulu kuhusu BBI

Raila Odinga amekuwa akisema kwamba hakuna muda wa kuifanyia marekebisho ripoti hiyo .

Muhtasari

 

  • Duru zaarifu kwamba  mkutano huo kati ya rais na naibu wake ulifanikishwa na mkutano ambao rais alikuwa amefanya na viongozi wa kidini siku ya jumanne .
  • Ruto  Ruto ametaka pawepo majadiliano Zaidi na kuhusishwa kwa  wote katika mchakato mzima wa BBI

 

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto

Rais Uhuru Kenyatta  siku ya jumatano amefanya mkutano uliodumu saa tatu na naibu wake William Ruto katika Ikulu ya Nairobi .

  Gazeti la The Star linaripoti kwamba mkutano huo ulikuwa kuhusu ripoti ya BBI  huku  masuala ambayo Ruto amekuwa akiyapinga katika ripoti hiyo yakiwa msingi wa mazungumzo kati ya viongozi hao  kabla ya hatua ifuatayo ya kundaa kura ya maoni kufanywa .

 Huku rais Kenyatta akishauri pawepo maelewano kuhusu baadhi ya mapendekezo yanayozua utata ,mshirika wake wa handshake Raila Odinga amekuwa akisema kwamba hakuna muda wa kuifanyia marekebisho ripoti hiyo .

 Duru zaarifu kwamba  mkutano huo kati ya rais na naibu wake ulifanikishwa na mkutano ambao rais alikuwa amefanya na viongozi wa kidini siku ya jumanne .

" Viongozi hao walimtaka rais ashirikiane na naibu wake ili kuhakikisha kwamba taifa haligawanywi kwa ajili ya mjadala kuhusu BBI’ duru zimeliarifu gazeti la The Star

 Viongozi hao wa kidini wamehofishwa na kinachoonekana kama kutengwa kwa Ruto katika mchakato mzima wa BBI na wameonya kwamba hatua hiyo inatshia kuligawanya tafa na kuzua mgogoro wa kisiasa .

" Wamemuarifu rais kwamba  Jinsi Ruto anavyoonekana kutengwa ndivyo ajenda yake ya kuliunganisha taifa inavyoonekana kuwa mazungumzo tu’

 Mkutano kati ya wawili hao umejiri pia siku ambayo kamati ya BBI imeahirisha  ghafla uzinduzi wa ukusanyaji wa saini za kufanikisha  kura ya maoni inayolenga kuirekebisha katiba .

Ruto  Ruto ametaka pawepo majadiliano Zaidi na kuhusishwa kwa  wote katika mchakato mzima wa BBI . Ameyataka mabunge ya  kaunti  kutotumiwa kuzua mgawanyiko utakaopelekea kura ya maoni itakayozua mirengo ya ‘Ndio’ na ‘la’.