Muhtasari
- Moto huo ulianza ijumaa alfajiri
- wafanyibiashara na zima moto wanaendelea kukabiliana na moto huo
Wafanyibiashara katika soko la Gikomba wanakadiria hasara kubwa waliopata baada ya moto mwingine kuzuka na kuteketeza sehemu ya soko hilo ijumaa alfajiri . maafisa wamesema chanzo cha moto huo hakijulikani . wafanyibiashara wameendelea kuuzima moto huo ulioanza mida ya alfajiri .
Zima moto kutoka kaunti ya jiji la nairob pia zimeelekea katika eneo hilo kusaidia katika juhudi za kuuzima moto huo.
Kumekuwa na msururu wa visa vya moto kuzuka katika soko hilo na kuwasababishia wafanyibiashara hasara ya mamilioni ya pesa .
Mnamo februari Mosi moto mwingine uliteketeza sehemu kuba ya soko hilo na kuwaacha hoi mamia ya wafanyibiashata . maafisa wa kaunti wameapa kufanya uchungiuzi kufahamu chanzo cha mikasa hiyo ya moto