- Anashtumiwa kwa kutumia vibaya pesa za chama na kukosa uwazi
- Aukot hata hivyo atasalia kuwa manachama wa Thirdway Alliance
Msajili wa vyama vya kisisasa ameidhinisha kuondolewa kwa Ekuru Aukot kama kiongozi wa chama cha Thirdaway Alliance.
Katika barua ya tarehe 18 Novemba mwaka huu iliyoandikiwa katibu mkuu wa chama hicho Fredrick Okango, msajili wa vyama Ann Nderitu amesema ofisi yake imeridhishwa na utaratibu wa kumuadhibu Aukot na kuondolewa kwake kutoka nafasi hiyo .
Amesema “ Chama kinashauriwa kutekeleza uamuzi wa baraza kuu kama inavyokubaliwa chini ya kipengee cha 14(k) cha katiba ya chama .
Hata hivyo Nderitu amesema uamuzi wa kumfurusha Aukot kama mwanachama haujaridhisha ofisi yake na hivyo basi kudinda kuishinisha uamuzi huo .
Aukot alifurushw akutoka chama hicho mwezi septemba kwa utumizi mbaya wa fedha na ukosefu w uwazo kwa wanachama wa Thirdway Alliance .
NE iliamua kumuondoa Aukot kama kiongozi wa chama hicho alipokataa kufika mbele ya kamati ya nidhamu .