Siasa za PEV ba 2022

Ruto: Kuzifufua kesi za ghasia za baada ya uchaguzi ni jaribio la kuleta uhasama wa kikabila

Kinoti amesema halengi kuzifufua kesi hozo

Muhtasari

 

  •  Ruto amesema jaribio hilo la Kinoti ni la kuzua uhsama wa kikabila 
  •  washirika wa Ruto wamemkashfu Kinoti kwa kukubali kutumiwa kisiasa 

 

Naibu wa rais William Ruto ametoa msimamo wake kuhusu kufufuliwa kwa kesi za  ghasia za baada ya uchaguzi akisema ni njama ya kuleta ukabila

" Jaribio lenye hila za kuzirejesha kesi hizo ni njama ya kufufua tena mradi wa ukabila’ amesema

 Kupitia twitter amesema ,mradi huo wa ukabila uliharibiwa na vugu vugu lake la mahasla  baada ua kugunduwa kwamba umaskini na ukosefu wa kazi umesababisha na uongozi mbaya na sio makabila ya humu nchini .

 Imeripotiwa kwamba serikali imeamua kuzifufua kesi za ghasia za baada  ya uchaguzi wa 2007/2008  huku waathiriwa wa kuteketezwa kwa kanisa la Kiambaa wakiwa tayari kutoa ushahidi .

 Hatua hiyo imejiri miaka saba baada ya serikali kusema haina ushahidi kuwachukulia hatua wanaodaiwa kuteleleza mauaji , uharibifu wa mali na machafuko baada ya uchaguzi huo .

 Wabunge Zaidi ya 40 wanaomuunga mkono naibu wa rais Ruto  wamemkashifu vikali mkuu wa DCI George Kinoti  kwa kuwa na nia ya kuzifugua kesi hizo .

 Wabunge hao wa tanga tanga wamemshtumu Kinoti kwa kujaribu kuchochea ghasia  miongoni mwa jamii zinazoishi Rift Valley .

 " Wanaomtumia Kinoti wamerejea ..ni wazi kwamba ana watu wanaomtuma kufanya hiki anachlenga kufanya kwa kuwatumia vibaya waathiriwa wa ghasia za uchaguzi ili  kuendeleza ajenda ya kisiasa’ amesema seneta wa Nakuru Susan Kihika

 Akiisoma taarifa ya wabunge hao  ,Kihika amedai kwamba Kinoti anatumiwa kuwalazimisha wakenya kuunga mkono Ripoti ya BBI  na kuthibiti siasa za urithi mwaka wa 2022 .

 Hata hivyo Kinoti amepuuza madai hayo akisema kwamba halengi kuzifufua kesi hizo .amesema kikao chake jana ni kuwahakikishia waathiriwa wa ghasia hizo na wakenya kwamba hapatatokea visa kama hivyo tena  na pia baada ya watu kadhaa kuripoti kutishwa .