Corona

Watu 6 wafariki huku 69 wakipatikana na corona

Leo wagonjwa 98 wamepona ugonjwa huo na kufikisha 77,521 watu waliopona ugonjwa huo .

Muhtasari
  • Leo wagonjwa 98 wamepona ugonjwa huo  na kufikisha 77,521  watu waliopona ugonjwa huo .
  • Hata hivyo watu sita wameaga dunia kwa ajili ya corona na kufikisha 1,664 idadi  ya watu walioangamizwa na Corona .
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

 Watu 69 wamepatikana na Corona  baada ya sampuli 1,987 kupimwa katika saa 24 zilizopita  na kufikisha 95,992  jumla ya idadi ya visa vya ugonjwa  huo nchini  huku  jumla ya sampuli zilizopimwa zikifika 1,035,309 .kutoka visa hivyo 53 ni wakenya ilhali 16 ni raia wa kigeni .40 ni wanaume ilhali wanawake ni 29.Mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa miaka mitatu ilhali wa umri wa juu ana miaka 86 .

Leo wagonjwa 98 wamepona ugonjwa huo  na kufikisha 77,521  watu waliopona ugonjwa huo .

Hata hivyo watu sita wameaga dunia kwa ajili ya corona na kufikisha 1,664 idadi  ya watu walioangamizwa na Corona .

 Kwa sasa  kuna wagonjwa 673 waliolazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini huku wengine 3,386 wakiwa chini ya mpango wa utunzi wa nyumbani . wagonjwa 34 wapo katika kitengo cha ICU ilhali 7 wapo HDU .