Baadhi ya washirika wa naibu wa rais William Ruto wamedai kwamba huenda akakitumia chama kingine kuwania urais mwaka wa 2022 .
Wakizungumza siku ya jumapili wamesema kwamba hatua ya kukibadilisha jina chama cha Party for Reforms and Development hadi United Democratic Alliance ni sehemu ya mpango huo wa kuhakikisha kwamba Ruto anapata makao mapya akiamua kuondoka Jubilee .
“ Tulikihama chama cha Jubilee kitambo sana .Sasa tupo chama kipya’ amesema mbunge mmoja aliye karibu na DP Ruto ambaye hakutaka kutambuliwa
Msajili wa vyama vya kisiasa siku ya jumatatu alitoa notisi ya nia ya kubadilisha jina la PDR hadi UDA na kuzua uvumi kwamba kambi ya Ruto imeshapata njia ya kupata chombo kipya cha kutumia kwa uchaguzi mkuu ujao endapo ataamua kuondoka Jubilee .
Katika arifa ya gazeti rasmi la serikali iliyochapishwa siku ya jumatatu ,chama hicho pia kinataka kubadilisha nembo yake kutoka fahali ili kuwa wheelbarrow na kauli mbiu ya ‘Kazi Ni Kazi’
Ruto na washirika wake wamejipata katika kipindi cha mvutano na uongozi wa chama cha Jubilee hasa kuhusiana na masuala makubwa kama vile kuwasimamisha wagombeaji katika chaguzi ndogo .huko msambweni ,mgombeaji huru aliyeungwa mkono na Ruto alimshinda mgombeaji wa chama cha ODM baada ya Jubilee kukosa kumsimamisha mgombeaji kwa sababu ya mwafaka wa handshake