Covid 19

106 wapatikana na Corona huku 1 akiaga dunia

Wagonjwa wengine 2,964 wapo chini ya mpango wa utunzi wa nyumbani .

Muhtasari
  • Wagonjwa 77 ni wanaume ilhali wanawake ni 29
  •  Leo watu 184 amepona ugonjwa huo na kufikisha 79,257 watu waliopona  Corona .

 Watu 106 wamepatikana na virusi vya Corona  baada ya sampuli 3,315 kupimwa katika saa 24 zilizopita  na kufikisha visa vya ugonjwa huo nchini hadi sasa kuwa 96,908.

 Idadi ya sampuli zilizopimwa sasa ni 1,059,006 .kutoka visa hivyo 97 ni wakenya ilhali 9 ni raia wa kigeni .mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa miezi tisa ilhali aliye na umri wa juu ana miaka 70 . Wagonjwa 77 ni wanaume ilhali wanawake ni 29

 Leo watu 184 amepona ugonjwa huo na kufikisha 79,257 watu waliopona  Corona .

 Hata hivyo mtu mmoja ameaga dunia na kufikisha 1,686 idadi ya waliofariki kutokana na virusi vya Corona . Kuna wagonjwa 617 waliolazwa katika hospitali mbali mbali nchini huku 28 wakiwa katika kitengo Cha ICU .Wagonjwa wengine 2,964 wapo chini ya mpango wa utunzi wa nyumbani .