Afisa wa Knut akosoa TSC kwa kusambaratisha Nato

Muhtasari

  • Mweka hazina alisema kwamba TSC inahujumu Knut.

  • Alisema vitendo vya TSC vilikuwa vinaathiri ari ya walimu.

 

Muweka Hazina wa Kitaifa wa mmuungano wa kutetea maslahi ya walimu nchini KNUT) John Matiang’i amekashifu tume ya kuajiri walimu (TSC) kwa kudhibiti uhuru wa kuabudu.

Matiang’i, ambaye alizungumza katika Uwanja wa Gusii siku ya Jumapili wakati akiongoza uchaguzi wa matawi alibainisha, kwamba hatua ya Tume ya TSC kupiga marufuku walimu kuhudhuria mafunzo, uchaguzi na shughuli zingine siku za wiki ni kinyume cha sheria.

Aliwaomba makasisi na wabunge kukemea agizo hilo akisema ni kinyume cha katiba.

"Viongozi wa kanisa na wanasiasa hawapaswi kusalia kimya  na kuwaacha washirika wao wakihujumiwa na mwajiri wao anaye kaidi Katiba," alibainisha.

“Walimu wananyimwa nafasi ya kuabudu kwa siku wanazopendelea kwa sababu lazima wahudhurie mafunzo mwishoni mwa wiki. Kama ilivyo sasa, tumelazimishwa kufanya uchaguzi Jumamosi na Jumapili wakati tunapaswa kuwa kanisani. Hatuwezi kukubali kufanya kazi wikendi, ”Matiang’i alisema.

Aliongeza: “TSC sasa imekuwa tume mbovu ambayo inatekeleza sera haramu na kuwatisha walimu. Tunaonya tume kwamba walimu watakataa aina yoyote ya vitisho. "

Alisema vitendo vya TSC vilikuwa vinaathiri ari ya walimu.

“Walimu wana ari ndogo na wanahisi kutishiwa. Barua za onyo zimekuwa kawaida. Unaweza kuchukua ng'ombe kwenye mto lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji, "aliongeza.

Matiang’i alizidi kuonya kuwa TSC inafanya juhudi kuangamiza knut.

 “Tulikuwa na wanachama zaidi ya 100,000 lakini idadi hii imepungua kwa sababu ya vitisho yva mwajiri wetu.

 KNUT haitakufa na ninataka kumwomba Rais Uhuru Kenyatta aingilie kati.

”aliwaambia wanachama kwamba wiki iliyopita, kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga aliuliza TSC na Chama cha Kitaifa cha Walimu Kenya (KNUT) kupata suluhisho la mzozo wao.

“la leo, uanachama wa Knut umepungua kutoka kiwango cha juu cha 187,000 hadi 23,000. Mapato yake yamepungua kutoka Shilingi milioni 144 hadi Shilingi milioni 15 dhidi ya gharama za takriban shilingi milioni 80 kwa mishahara ya zaidi ya wafanyikazi 600 walioenea kote nchini, ”Raila alisema.