Mauaji ya kinyama Kiambu: Familia ya mfanyakazi inaomba msaada wa kumzika

Muhtasari
  • Familia ya mfanyakazi aliyeuawa Kiambu yaomba msaada wa kupanga mazishi na kulipa gharama ya hospitali
  • Binamu yake alisema kwamba kifo cha ndugu yake hakipwi kipaumbele licha ya yake kuwaacha watoto wawili wakiwa mayatima

Binamu yake mfanyakazi aliyeuawa katika mauaji ya kinyamaKiambaa kaunti ya Kiambu Elizabeth Kinyajui ameomba msaada ili waweze kumzika KInyanjui Wambaa.

Huku akizungumza siku ya Jumatatu Binamu huyo alisema kwamba mauaji ya binamu yake hayajapewa kipaumbele.

"Naona tu ndugu yangu akiitwa mkulima, mfanyakazi wa ujenzi, ni mwanadamu pia, mwenye familia." Alisema Elizabeth.

 

Elizabeth alisema kwamba wanaomba msaada kutoka kwa wasamiria wema kulipa gharama ya hospitali na kupata pesa ya kupanga mazishi yake.

Kinyanjui,38 alikuwa baba wa watoto wawili.

Lawrence ambaye alikiri kuangamiza familia yake alipelekwa mbele ya mahakama siku ya Jumatatu ili kujibu mashtaka.

Mpenzi wake pia alikuwa mbele ya mahakama, ambapo wapelelezi walipewa siku 14 kufanya na kumaliza uchunguzi.

Kinachowashangaza wananchi na jamaa je Lawrence alitekeleza mauaji hayo peke yake jinsi alivyodai?

Washukiwa hao watasalia korokoroni kwa siku 14.

Pia Elizabeth alisema kwamba nyumba yake imefungwa na mwenye nyumba kwa maana hajalipa kodi licha ya yake kuwa na watoto.