Mauaji ya Kiambu: Silaha za mauaji za patikana huku muuaji akikiri kutekeleza mauaji hayo

Muhtasari
  • Silaha za mauaji za patikana huku muuaji akikiri kutekeleza mauaji hayo baada ya kuwapeleka wapepelezi alipokuwa ameficha silaha alizotumia
  • Mpenzi wake Lawrence pia yuko mikononi mwa polisi kwa uchunguzi

Mwana wa kiume wa jamaa aliyeuawa kinyama pamoja na mkewe na wanawe wengine wawili katika eneo la Karura kaunti ya Kiambu akiri kuwauawa wazazi wake na ndugu zake wawili huku akielekeza maafisa wa upelelezi Mai Mahiu alipokuwa ameficha silaha alizotumia kutekeleza kitendo hicho.

Lawrence Waruinge,23 mwanafunzi wa chuo kikuu alitiwa mbaroni siku ya Ijumaa baada ya kutoweka na kuenda mafichoni.

Baada ya kukamatwa alikiri kutekeleza mauaji hayo huku akiwapeleka maafisa wa polisi alipokuwa ameficha silaha za mauaji hayo.

Alikuwa ameficha silaha hizo kwenye shimo ya choo, polisi walichimba shimo hilo na kupata silaha kama Kisu,viatu, na karatasi.

Pia aliwapeleka maafisa hao mahali alipochoma baadhi ya silaha nyingine ambazo alitumia kuwauwa wazazi wake na ndugu zake na mfanyakazi wa boma lao.

Polisi walisema kwamba Lawrence alikiri kuwauwa watano hao pekeyake.

Lakini polisi walisema kwamba kuna uwezekano kwamba Lawrence hakutekeleza mauaji hayo pekeyake bali alikuwa na watu wengine.

Jambo la kushangaza ni pale mshukiwa huyo alisema jinsi alikabiliana na baba yake mzazi kabla ya kumdunga.

Lawrence alidai kwamba alimshika baba yake baada ya kuvunja mguu wake alipokuwa anamkimbia, ndiposa akapata fursa ya kumshika na kumdunga.

"Alisema baba yake alipigwa na umeme na kuruka kutoka kwa ghorofa ambapo alivunjika mguu, hii ilimpa muda wa kumfikia baba yake na kumuua kama nyoka." Alisema Polisi aliyesikia Lawrence akikiri.

Mwili wa baba yake ulikuwa na majeraha 34 ya kudungwa.

Mpenziye Larence ambaye alikuwa anaishi naye eneo la Mai Mahiu pia naye yuko mikononi mwa polisi kwa uchunguzi zaidi.

Baada ya kuwauwa watano hao akitumia kisu mwendo wa saa mbili usiku, Lawrence alienda katika soko la Wangige akitumia pikipiki.

Baada ya kufika hapo alichukua gari la abiria na kuelekea Mai Mahiu huku akiwa amebeba silaha alizotumia kutekeleza mauaji hayo.

Mwana bodaboda huyo yuko bado kutiwa mbaroni kwa uchunguzi na maswali zaidi.