Uhasama

‘Bifu’ kati ya Sonko na Kibicho imekuwa ikiendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja

Baadaye Sonko tena aliibuka na madai mengine ya kunyanyaswa na polisi waliokuwa wakipewa maelekezo na Kibicho

Muhtasari
  •  Baadaye Sonko tena aliibuka na madai mengine ya kunyanyaswa na polisi waliokuwa wakipewa maelekezo na Kibicho
  • Madai hayo yalimfanya Kibicho kwenda katika makao makuu ya DCI  ili kuandikisha  taarifa .

 

Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko(Kushoto) na Katibu wa kudumu wa usalama wa ndani Karanja Kibicho(Kulia)

Malumbano kati ya gavana wa zamani wa Nairobi  Mike Sonko na katibu wa kudumu wa wizara ya usalama wa ndani Karanja Kibicho yamekuwepo kwa Zaidi ya mwaka mmoja sasa  

 Sonko ambaye amejipa weledi wa kupaua mbarika kuhusu masuala mazito mazito ya taifa na serikali  amekuwa akiliingiza jina la Kibicho katika kila sakata na hata kumlaumu kwa baadhi ya maamuzi ya serikali kuu .

 Wakati mmoja katika mahojiano ya runinga Sonko alimtaja Kibicho kama  ‘Deep State’-Kuashiria watu na taasisi zenye maamlaka zinazofanya maamuzi bila kufuata mkondo wa sheria na utawala kama kama  inavyofaa .

 Katika jaribio la kwanza la kumtoa Sonko madarakani kupitia kura ya kutokuwa na Imani naye ilidaiwa kwamba waakilshi waliokuwa wakimpinga Sonko alikuwa wakipigwa jeki na fia moja mkuu wa serikali mwenye ushawishi mkubwa .

 Baadaye Sonko tena aliibuka na madai mengine ya kunyanyaswa na polisi waliokuwa wakipewa maelekezo na Kibicho . Alikuwa amewashtumu polisi kwa kuhujumu  jitihada zake za kukabiliana na janga la Corona   baada ya kuleta mashine maalum za kufikiza dawa  katikati mwa jiji ambazo ziliharibiwa .

  Mwishoni mwa wiki Sonko alidai kwamba yeye pamoja na Kibicho na watu wnegine ambao hakuwataja walinunua magari na kuyachoma wakati wa kampeini za uchaguzi uliopita ili kukisingizia chama cha ODM Na kiongozi wake Raila Odinga kwa kusababisha ghasia . Madai hayo yalimfanya Kibicho kwenda katika makao makuu ya DCI  ili kuandikisha  taarifa .