Hakimu adinda kujiondoa kwenye kesi ya Sonko

Muhtasari

• Ogoti siku ya Alhamisi alipuuzilia mbali madai ya upendeleo kama yaliyotolewa na Sonko.

 Hakimu Mkuu wa mahakama ya Kupambana na Ufisadi Douglas Ogoti amedinda kujiondoa kutoka kwa kesi ya shilingi milioni 10 inayo mkabulialiyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko na washtakiwa wengine.

Ogoti siku ya Alhamisi alipuuzilia mbali madai ya upendeleo kama yaliyotolewa na Sonko.

Hata hivyo, Ogoti alisema hakuna ushahidi wa upendeleo wa kibinafsi umeonyeshwa dhidi ya korti.

Alisema pia hakuna ushahidi kwamba sababu zingine zilikuwa zimeathiri maamuzi ya mapema ambayo ametoa katika kesi hiyo.

Ogoti pia alisema hakukuwa na ushahidi kwamba matamko ya korti hii katika maamuzi mengine ya mapema, katika kesi hii, yana ushawishi wa kibaguzi.

Ogoti alisema Sonko lazima aonyeshe sababu za kibinafsi au sababu za ziada kwa korti kujiondoa.

"Sioni uthibitisho wowote wa upendeleo. Maombi ya Sonko hayana msingi na yametupiliwa mbali," aliamua.

Ogoti pia aliamua kwamba kesi hiyo lazima iendelee bila kujali uwakilishi.

"Mtuhumiwa alipewa muda kuthibitisha madai yao. Korti hii ilijaribu kila iwezelo kubaini madai bila mafanikio," alisema.