Hakimu aliyefutwa kazi miaka 10 iliyopitwa arejeshwa kazini

Muhtasari

• Mahakama ya rufaa siku ya Ijumaa ilimrejeshea Joseph Ndururi kwa nafasi yake ya zamani kama Hakimu Mkuu.

Hakimu ambaye alifutwa kazi miaka miwili iliyopita kwa madai ya utovu wa nidhamu amerejeshwa kazini.

Mahakama ya rufaa siku ya Ijumaa ilimrejeshea Joseph Ndururi kwa nafasi yake ya zamani kama Hakimu Mkuu.

Katika kesi hiyo tume ya huduma kwa mahakama (JSC) ilikuwa imekata rufaa uamuzi wa mahakama ya Leba kumpa Ndururi mshahara wa miezi 10 kwa kufukuzwa kazi kinyume cha sheria.

Hata hivyo, mahakama ya rufaa iliondoa tuzo hiyo na badala yake ikamrudishia kazi hiyo.

"Hakimu alisimamishwa kunyimwa haki zake na ilhali hakuchangia kwa njia yoyote kusimamishwa kwake kazi,” Mahakama iliamua.

Majaji Gatembu Kairu, Agnes Murgor na Wanjiku Karanja walishikilia zaidi kuwa hakimu alikuwa ametumikia kwa miaka 15 na kupata uzoefu kabla ya kutimuliwa kwa hivyo kunaweza kuwa hakuna fursa kwake kupata kazi nyingine.

"Mahakama ni taasisi kubwa kwa kweli ni mkono mzima wa serikali na mahakama zinahitaji wafanyikazi, Ndururi inaweza kupelekwa kutumikia katika mahakama hizo" majaji waliamua.

"Mtuhumiwa anarejeshwa katika ajira yake mara moja kwa ofisi ya Hakimu Mkuu bila kupoteza mshahara wa malipo ya nyuma na marupurupu" waliamua.

Majaji hao walibaini kuwa madai yaliyompeleka nyumbani yalisemekana kutekelezwa zaidi ya miaka 10, mapema mwaka 2006 na hakuchukia JSC kwani alikuwa ameendelea kuhudumu katika nyadhifa kadhaa kabla ya kufutwa kazi.