Mvua kuendelea katika maeneo mengi ya nchini wiki hii

Muhtasari

• Sehemu zingine katika Nyanda za Juu Mashariki mwa Bonde la Ufa pamoja na Nairobi zitapokea mvua Jumanne, Jumatano na Jumapili.

• Mvua kubwa inayoendelea katika eneo la Pwani ilisababisha mafuriko siku ya Jumatatu, na kuharibu sehemu ya barabara ya Garissa-Garsen.

Wenye magari wanaotumia barabara kuu ya Garissa-Hola-Garsen waliathirika sana siku ya Jumatatu kutokana na mvua kubwa
Wenye magari wanaotumia barabara kuu ya Garissa-Hola-Garsen waliathirika sana siku ya Jumatatu kutokana na mvua kubwa
Image: KENHA

Wataalamu wa hali ya hewa wamedokeza kwamba maeneo mengi za nchi yataendelea kupokea mvua katika siku saba zijazo, ingawa kiwango cha mvua kinatarajiwa kupungua kadiri kipindi cha utabiri kinapoendelea.

Maeneo machache kaskazini magharibi na kaskazini mashariki yana uwezekano mkubwa kupata upepo mkali wa kusini-mashariki na kasi inayozidi kilomita 46.3 kwa saa.

Katika kipindi cha utabiri, kaunti za Siaya, Kisumu, Homabay, Kisii, Nyamira, Trans Nzoia, Baringo, Uasin Gishu, Elgeyo Marakwet, Nakuru, Narok, Kericho, Bomet, Kakamega, Bungoma na Busia zitapokea mvua za asubuhi Jumanne na Jumatano.

Mvua za jioni zinatarajiwa katika maeneo machache katika kipindi chote cha utabiri.

Kaunti za Turkana, Pokot Magharibi, na Samburu pia zitapata mvua za asubuhi Jumanne, Jumatano, na Jumapili na asubuhi zingine zinaweza kuwa na jua.

Mvua za alasiri na ngurumo za radi  zinaweza kutokea katika maeneo kadhaa Jumanne na juu ya maeneo machache Jumatano na Jumapili katika maeneo ya Kaskazini Magharibi.

Sehemu zingine katika Nyanda za Juu Mashariki mwa Bonde la Ufa pamoja na Nairobi zitapokea mvua Jumanne, Jumatano na Jumapili.

Mvua za alasiri pia zinaweza kutokea katika wa maeneo kadhaa Jumanne, Jumatano, na Alhamisi.

Mvua za asubuhi zitapatikana katika nyanda za kusini-mashariki Jumanne na Alhamisi wakati asubuhi zingine zinaweza kubaki na jua.

Eneo la ukanda wa Pwani litapokea mvua Jumanne asubuhi na maeneo machache Jumatano.

Katika siku saba zilizopita, mvua ilirekodiwa katika sehemu kadhaa za nchi.

Ikilinganisha viwango vya mvua kipicha cha awali (Machi 22-28) na kipindi cha sasa (Machi 29-Aprili 4) kunaongezeko kubwa la kiwango cha mvua katika sehemu nyingi za nchi.

Mvua kubwa inayoendelea katika eneo la Pwani ilisababisha mafuriko siku ya Jumatatu, na kuharibu sehemu ya barabara ya Garissa-Garsen.

Mvua kubwa pia imesababisha mafuriko katika maeneo tambarare ya Bura.

Mamlaka ya Barabara Kuu ya Kenya ilikuwa imehamasisha wahandisi wake na kontrakta kutathmini kiwango cha uharibifu ambao uliathiri waendesha magari wanaotumia barabara ya Garissa-Hola-Garsen.