MADOWO ARUDI NCHINI

Madowo aajiriwa na CNN

Madowo atakuwa akiripotia eneo la AfriKa Mashariki akiwa mjini Nairobi.

Muhtasari

•Hapo awali amekuwa KTN, NTV na CNBC

•Asema ni furaha yake kurudi Kenya.

Mwanahabari Larry Madowo
Mwanahabari Larry Madowo

Mwanahabari mashuhuri  Larry Madowo anatarajiwa kurejea nchini Kenya baada yake kuajiriwa na Kampuni ya CNN.

Mwanahabari huyo mzaliwa wa mkoa wa Nyanza nchini Kenya ataifanyia kazi kampuni hiyo ya kimataifa  akiiripotia toka upande wa Nairobi, Kenya.

Hivi karibuni, Madowo amekuwa kwenye  kampuni  ya uanahabari  tajika  ya BBC akiripotia pande ya Washington DC iliyoko Amerika ya Kaskazini.

 

Akitoa tangazo hilo, Deborah Rayner ambaye ni mmoja wa wakuu katika CNN amemsifia Larry kama mwanahabari shupavu na aliye na uzoefu mkubwa katika kazi ya uanahabari.

“Larry ana utaalamu mkubwa mno kwenye ripoti katika ulingo wa siasa,  biashara, sekta ya burudani na yanayojiri.  Atatusaidia sana kuripoti yanayotokea upande wa Africa Mashariki na kukiuka” Bi Rayner alisema.

Kwa upande wake Madowo alidai kuwa kurudi Kenya ni furaha yake hususan wakati  wa huu muhimu.

“Nina furaha sana kujiunga na timu hii shupavu  ya CNN. Nimependezwa sana na kazi yao kubwa ya kupongezwa ambayo CNN imekuwa ikifanya,” Madowo alisisitiza.

Madowo alianza kazi yake ya uanahabari hapa Kenya akiripotia stesheni ya KTN kisha akahamia NTV kabla yake kupata kazi na CNBC Africa huko Afrika Kusini ingawa hakukaa sana kabla yake kupata ajira katika shirika  la BBC huko America.

Ameifanyia BBC kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja.