Meli ya BBI yazama! Mahakama yapuuzilia mbali mchakato mzima wa BBI

Muhtasari

• Mahakama ilikosoa hatua ya rais Uhuru Kenyatta kuongoza mchakato wa marekebisho ya katiba wakisema kwamba shughuli hiyo inafaa kumilikiwa na wananchi na wala sio rais .

• Majaji walikosoa pendekezo la BBI kubuni maeneo bunge mapya sabini wakishikilia kwamba jukumu hilo ni la tume ya uchaguzi na mipaka na sio la jopo ya lililoteuliwa na rais Kenyatta.

Rais Uhuru Kenyatta
Image: PSU

Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga wamepata pigo kubwa katika azma yao ya kufanyia mabadiliko katiba baada ya mahakama kupuuzilia mbali mchakato mzima wa BBI.

Jopo la majaji watano Joel Ngugi, George Odunga, Jarius Ngaah, Janet Mulwa na Chacha Mwita siku ya Alhamisi jioni walitoa uamuzi wa kijasiri kwamba mchakato wa kubadilisha katiba kuanzia kwa jopo lililoteuliwa na rais Uhuru Kenyatta yote yalifanywa kinyume na sheria.

Kulingana na uamuzi huo wa mahakama uliosomwa kwa takriban saa saba  majaji hao watano walikosoa hatua ya rais Uhuru Kenyatta kuongoza mchakato wa marekebisho ya katiba wakisema kwamba shughuli hiyo inafaa kumilikiwa na wananchi na wala sio rais .

Pia walikosoa rais Kenyatta kwa kuteua jopo maalum kuongoza zoezi la marekebisho ya katiba wakisema kwamba hatua hiyo ilikuwa kinyume na katiba ya Kenya.

Majaji hao walisema kwamba jopo lililoteuliwa na rais Uhuru Kenyatta halikuwa na mamlaka ya kusimamia shughuli ya marekebisho ya katiba.

Kuhusu tume ya uchaguzi na mipaka IIEBC mahakama ilisema kwamba tume hiyo haina idadi ya kutosha ya makamishna kufanya uamuzi wowote unaoathiri sera kuu za taifa.

Tume ya uchaguzi kwa sasa ina makamishna watatu pekee kufuatia kujiuzuku kwa jumla ya makamishna wanne.

Mahakama pia ilisema kwamba baadhi ya mapendekezo ya muswadi wa marekebisho ya katiba yanakwenda kinyume na sheria. Walikosoa pendekezo la BBI kubuni maeneo bunge mapya sabini wakishikilia kwamba jukumu hilo ni la tume ya uchaguzi na mipaka na sio la jopo ya lililoteuliwa na rais Kenyatta.

Makama ilitamaitisha kauli yake kwa kusema kwamba mabadilko ya katiba yanayoshinikizwa chini ya mwafaka wa BBI sio ya wananchi bali ni mchakato unaongozwa na Uhuru Kenyatta.

Mahakama pia ilionya maafisa wa serikali dhidi ya kutumia raslimali za umma kuendeleza shughuli hiyo ambayo ni kinyume cha katiba.

 

Punde tu baada ya mahakama kutoa uamuzi kuhusu mchapkati wa BBI naibu rais William Ruto aliandika kwenye Twitter akisema kwamba .... "Kuna MUNGU mbinguni anayependa kenya bila kipimo. Jina la MUNGU lisifiwe milele."

 

Mnamo Februari, BBI ilipata pigo kubwa baada ya Mahakama Kuu kuizuia IEBC kuanzisha mipango ya kura ya maamuzi kuhusu Muswada wa marekebisho katiba, 2020.

Katika uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watano, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilisimamishwa kwa muda kujiandaa kwa kura ya maamuzi ili kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa maombi saba yaliyowasilishwa kupinga mchakato huo.

Majaji walikuwa wameonya bunge la kitaifa, seneti na mabunge ya kaunti dhidi ya kuharakisha mchakato wa BBI.

Muswada wa marekebisho ya katiba (2020) maarufu kama muswada wa BBI ulikuwa tayari umeidhinishwa na mabinge yote mawili ya kitaifa pamoja na mabunge ya kaunti na ulikuwa ukabidhiwe rais Uhuru Kenyatta ambaye angeuwasilisha kwa tume ya IEBC kuandaa kura ya maamuzi.

Inatarajiwa kwamba upande wa seriali ukiongozwa na mwanasheria mkuu utawasilisha rufaa dhidi ya umauzi huo.