Mfanyabiashara Chris Kirubi kuzikwa Jumamosi Thika

Muhtasari
  • Mfanyabiashara Chris Kirubi kuzikwa nyumbani Jumamosi
  • Mfanyabiashara maarufu marehemu atazikwa kwenye shamba lake huko Thika Jumamosi

Ibada ya wafu ya marehemu mfanyabiashara wa Kenya Dkt Chris Kirubi itafanyika Ijumaa katika kanisa la Faith Evangelistic Ministry (FEM) huko Karen, Nairobi, kuanzia saa tano asubuhi.

kulingana na taarifa kutoka kwa kamati ya maandalizi wageni watakao hudhuria hafla hiyo wanaombwa kuwa wameketi saa nne unusu.

Mfanyabiashara maarufu marehemu atazikwa kwenye shamba lake huko Thika Jumamosi.

Chris Kirubi, auDJ CK kama alivyojulikana sana, alikufa saa saba  Jumatatu, Juni 14, akiwa na umri wa miaka 80 baada ya kupigana na saratani kwa muda mrefu.