Muigizaji adai kuzuiwa kumzika baba watoto, Benjamin Ayimba

Muhtasari

• Moraa alisema alikutana na Ayimba wiki kadhaa baada ya kuachana na mumewe wa kwanza wa miaka saba.

• Anajuta kwamba familia ya Ayimba haikumuunga mkono.

MSANII NYABOKE MORAA
MSANII NYABOKE MORAA

TAARIFA YA ELIZABETH NGIGI 

Aliyekuwa mwigizaji wa zamani wa kipindi cha Tahidi High Nyaboke Moraa anasema alizuiwa kumzika babaake mtoto wake mkufunzi wa zamani wa timu ya taifa ya raga ya Kenya Benjamin Ayimba na dada yake Ayimba.

Akihojiwa kwenye Radio Jambo na Massawe Japanni, Moraa alielezea tofauti zilizoibuka baada ya kifo cha Ayimba wiki chache zilizopita.

Moraa alisema alikutana na Ayimba wiki kadhaa baada ya kuachana na mumewe wa kwanza wa miaka saba.

Walipendana na kuishi pamoja kwa miaka minane kabla ya kutengana mwaka 2018 wakiwa na watoto wawili.

"Alinijia na mwanzoni nilikataa kwani nilikuwa nimetengana tu na bwanangu wa kwanza," alisema.

Moraa alisema alidhani alikuwa mke wake wa pili lakini ikawa ni mke namba tatu.

"Ana watoto kama kumi na wanawake tofauti. Upendo wetu ulikuwa sawa lakini tulikuwa na changamoto kadhaa na baada ya miaka minane, karibu na 2018, tulitengana," alisema.

Kile ambacho kilifuata ni vita kali vya ulezi kati ya wawili hao ambavyo vilileta uhasama baina yake na familia ya Ayimba.

"Kulikuwa na polisi 30 kwenye kiwanja wakati wa mazishi. Waliniuliza nilikuwa nikifanya nini huko. Nilisema nilikuwa nimeleta watoto wangu kuaga baba yao. Unajua watoto wangu walikuwa wakiniuliza ikiwa tutakwenda kanisani kumuona baba, "alisema.

"Baada ya kusukumana na kushinikiza langoni, polisi walituruhusu kuingia. Nilikwenda hemani, nilikuwa dhaifu sana wakati huo. Watu wengine walikuwa wakisema mimi ndiye niliyemuua. Polisi waliambiwa naja kusababisha machafuko, lakini hakukuwa na pesa za kupigania. "

Anajuta kwamba familia ya Ayimba haikumuunga mkono.

"Nimewahi kwenda nyumbani kwa Ayimba mara tatu hapo awali. Mama na baba yake hawakusema chochote ingawa waliona kile nilichopitia. Nimeishi na watu hawa kwa muda mrefu na hata niliishi na mmoja wa watoto wa Ayimba kwa miaka ninane bado wao hawakunitetea. "

"Tulitaka kupiga picha kaburini baada ya kuzikwa lakini watoto wangu awali walizuiliwa. Dada ya Ayimba aliwaita watoto wangu Chokoras (watoto wa mitaani) na 'mistakes'. Alininyanyasa sana.

Lakini nimemsamehe "Moraa alimtaja marehemu Ayimba kama mtu mwenye upendo.

(Imetafsiriwa na kuhaririwa na Davis Ojiambo).