Airtel yaongeza ada ya kupiga simu

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Prasanta Da Sarma amesema kuwa mabadiliko hayo yamechangiwa na kuongezewa kwa ushuru wa huduma za simu kutoka 15% hadi 20%.

Muhtasari

•Kampuni ya huduma za simu, Airtel Kenya imeongeza ada ya kupiga simu kwa huduma yoyote hadi shilingi 2.78.

•Hata hivyo, Sarma alisema kuwa ada ya data zinazotumika kuingia mtandaoni hazijabadilika.

Image: AIRTEL

Kampuni ya huduma za simu, Airtel Kenya imeongeza ada ya kupiga simu kwa huduma yoyote hadi shilingi 2.78.

Hii ni senti 78 juu ya ada iliyokuwepo hapo awali ya shilingi mbili.

Kupitia ujumbe uliotolewa asubuhi ya Ijumaa, mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Prasanta Da Sarma amesema kuwa mabadiliko hayo yamechangiwa na kuongezewa kwa ushuru wa huduma za simu kutoka 15% hadi 20%.

Watumizi wa huduma ya Airtel watalipia shilingi 2.78 kupiga simu kwa huduma yoyote kuanzia Ijumaa, Julai 2.

Hata hivyo, Sarma alisema kuwa ada ya kutuma jumbe na  ya data zinazotumika kuingia mtandaoni hazijabadilika. Huduma za Amazing, UnlimiNET na Tubonge bundles hazitabadilika.

"Tumejitolea kuhakikisha kuwa wateja wetu wanaendelea kufurahia thamani nzuri ya pesa zao kupitia huduma zetu" Sarma alisema.