Makali ya corona:Watu 595 wamepona corona,8 waaga dunia,431 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Kenya imesajili visa vipya 431 vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 5,281 chini ya saa 24 zilizopita
  • Visa hivyo sasa vinafikisha maambukizi ya Corona nchini Kenya hadi 193,189 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 8.2%
Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Kenya imesajili visa vipya 431 vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 5,281 chini ya saa 24 zilizopita.

Visa hivyo sasa vinafikisha maambukizi ya Corona nchini Kenya hadi 193,189 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 8.2%.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 416  ni wakenya ilhali 15 ni raia wa kigeni,284 ni wanaume huku 123 wakiwa wanawake.

Kulingana na wizara ya afya watu 8 wameaga dunia kutokana na viruis vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 3,783 ya walioaga dunia.

Jumla ya wagonjwa 595 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 182,921.542 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 53 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,224 ambao wamelazwa hospitalini,4,358 wamejitenga nyumbani.

Pia kuna wagonjwa 134 kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).