Mwanafunzi wa kike ajitia kitanzi

Muhtasari

• Polisi wanasema walifahamishwa kuhusu kisa hicho saa kadha baada ya msichana huyo kudaiwa kujiua.

crime scene
crime scene

Polisi wanachunguza kisa ambapo msichana mmoja alifariki baada ya kudaiwa kujiua ndani ya hosteli katika eneo la Alsops, Nairobi.

Bado haijabainika nini haswa kilimsukuma mwanamke huyo aliyekuwa katika miaka ya ishirini kujitoa uhai.

 Mwili wake uligunduliwa siku ya Alhamisi.

 Polisi wanasema walifahamishwa kuhusu kisa hicho saa kadha baada ya msichana huyo kudaiwa kujiua.

Marehemu anasemekana alikuwa mwanafunzi katika chuo kimoja katika eneo la Alsops.

Mwili ulichukuliwa kutoka eneo la tukio na kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti.

Familia yake hata hivyo imehojia hatua ya kuarifiwa kuhusu kifo chake muda mrefu baadaye na hata kuitwa kwa eneo la tukio kabla ya mwili kuhamishwa.

Polisi walisema shughuli ya kuufanyia mwili huo upasuaji kubaini kilichomuua imepangwa na matokeo yake yatachangia katika uchunguzi.