Covid-19: Watu 170 wapatikana na corona,254 wapona,1 aaga dunia

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 250,898 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.8 %
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,598,772
Image: HISANI

Kenya imesajili visa 170 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 6,162 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 158 ni wakenya ilhali 12 ni raia wa kigeni,83 ni wanaume huku 86 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 250,898 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.8 %.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,598,772.

Vile vile watu 254 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 243,591,216 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 38 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Hata hivyo mtu 1 ameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,179 ya walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 841 ambao wamelazwa hospitalini, 1,833 wamejitenga nyumbani.

HUku hayo yakijiri kuna wagonjwa 51 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).