Afueni kwa wasafiri baada ya serikali kutangaza kurejea tena kwa safari za usiku

Muhtasari

•Macharia amesema kwamba serikali itaendelea kuhimiza umma kuzingatia mikakati iliyowekwa na wizara ya afya kuthibiti maambukizi ya Corona.

Waziri James Macharia
Waziri James Macharia
Image: WANGECHI WANG'ONDU

Wasafiri wanaopenda kusafiri usiku hatimaye  wamepata afueni baada ya waziri wa usafiri James Macharia kutangaza kufunguliwa kwa safari za usiku.

Kupitia kwa ujumbe uliotolewa siku ya Ijumaa, Macharia amesema kwamba serikali itaendelea kuhimiza umma kuzingatia mikakati iliyowekwa na wizara ya afya kuthibiti maambukizi ya Corona.

Machari  amesema kwamba hatua hiyo itaboresha juhudi za serikali za kufufua uchumi na kuhakikisha kwamba wananchi wote wamechajwa.

"Nashukuru uongozi na wafanyikazi wote katika sekta ya usafiri kwa kujitolea kuunga serikali mkono katika kudhibiti maambukizi ya maradhi ya Corona" Macharia alisema.

Haya yanajiri siku mbili tu baada ya rais Uhuru Kenyatta kuondoa kafyu ya kitaifa ambayo ilikuwepo kwa kipindi cha zaidi ya miezi 18.