Kenya yafunga mpaka wake na Ethiopia kufuatia mapigano yanayoendelea nchini humo

Muhtasari

•Nduru za kuaminika zinasema kuwa jeshi la Kenya limepiga hatua ya kuzidisha doria kwenye mpaka wa kilomita 800 ili kuzuia wahamiaji haramu kuingia nchini.

Wapiganaji wa Tigray wamefanikiwa kudhibiti maeneo mengi ya jimbo hilo tangu mwezi Juni
Wapiganaji wa Tigray wamefanikiwa kudhibiti maeneo mengi ya jimbo hilo tangu mwezi Juni
Image: GETTY IMAGES

Kenya imefunga mpaka wake na Ethiopia kwa muda usiojulikana huku ghasia zikiwa zimekithiri katika nchi hiyo jirani upande wa kaskazini.

Nduru za kuaminika zinasema kuwa jeshi la Kenya limepiga hatua ya kuzidisha doria kwenye mpaka wa kilomita 800 ili kuzuia wahamiaji haramu kuingia nchini.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya serikali ya Ethiopia kutangaza hali ya hatari huku vita vikienea katika majimbo kadhaa nchini humo.

Serikali awali ilikuwa imewataka wakaazi katika mji mkuu wa Addis Ababa kujihami , huku waasi kutoka kaskazini mwa Tigray wakisonga mbele kuelekea eneo la kusini.

Inakadiriwa kuwa kuna uwezekano ya mamilioni ya raia  wa Ethiopia kukimbia nchi hiyo iwapo mapigano yataeendelea na kusababisha kuanguka kwa utawala.

Kenya ni baadhi ya nchi ambazo wahamiaji wanatarajiwa kujaribu kuingia huku serikali ikishauriwa kuwa macho.