Majambazi wasiojulikana wauwa abiria 6 Marsabit, 11 wajeruhiwa

Muhtasari

•Genge la majambazi waliokuwa wamejihami kwa bunduki lilishambulia lori ambalo lilikuwa limebeba abiria kutoka mji  wa Marsabit kuelekea Bardassa Manyatta.

•Majambazi hao walipiga abiria 17 risasi ambapo sita kati yao walipoteza maisha papo hapo huku wengine 11 waliojeruhiwa wakikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.

crime scene 1
crime scene 1

Watu sita waliuawa kwa kupigwa risasi na majambazi wasiojulikana jioni ya Alhamisi katika kaunti ya Marsabit.

Huduma ya polisi nchini (NPS) imeripoti kuwa watu wengine 11 waliachwa na majeraha ya risasi kwenye tukio hilo lililotokea mwendo wa saa kumi na mbili jioni.

Kulingana na polisi, genge la majambazi waliokuwa wamejihami kwa bunduki lilishambulia lori ambalo lilikuwa limebeba abiria kutoka mji  wa Marsabit kuelekea Bardassa Manyatta.

Majambazi hao walipiga abiria 17 risasi ambapo sita kati yao walipoteza maisha papo hapo huku wengine 11 waliojeruhiwa wakikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.

Majambazi wale wenye roho ya mnyama wanaripotiwa kutoroka punde baada ya kutekeleza mashambulio hayo huku juhudi za kuwasaka zikiwa zimekita mizizi.