Makali ya corona: Watu 61 wapatikana na corona,59 wapona

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,276  na kiwango cha maambukizi cha asilimia 1.1%
  •  
    Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,767,353
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Kenya siku ya JUmamosi imesajili visa 61 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 5,525 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 57 ni wakenya huku 4 wakiwa ni raia wa kigeni,36 ni wanaume huku 25 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,276  na kiwango cha maambukizi cha asilimia 1.1%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,767,353.

Aidha watu 59 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 247,633,43 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 16 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 390 ambao wamelazwa hospitalini, 1,038 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 27 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 5,974,566.