Rais Kenyatta amfuta kazi mkuu wa magereza baada ya wafungwa wa ugaidi kutoroka Kamiti

Muhtasari
  • Wycliffe Ogallo, Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza, amefutwa kazi
Wycliffe Ogalo
Image: Felix Kipkemoi

Wycliffe Ogallo, Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza, amefutwa kazi.

Rais Uhuru Kenyatta alimfuta kazi Ogallo Jumatano na kumteua Brigedia (Mst) John Warioba kuchukua nafasi yake.

Mabadiliko hayo yanafuatia kutoroka kwa hivi majuzi kwa wafungwa watatu wa ugaidi katika gereza la Kamiti Maximum.

"Mheshimiwa Rais leo amemteua na kushuhudia kuapishwa kwa Brigedia (Mst) John Kibaso Warioba kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza," taarifa kutoka Ikulu ilisema.

"Inaarifiwa pia kwamba Mheshimiwa Rais mapema leo alikuwa amebatilisha uteuzi wa Bw Wycliffe Ogalo kama Kamishna-Jenerali wa Kenya."