Mandago ampuuza Sudi asisitiza kuwania useneta

Muhtasari

• Mandago siku ya Jumanne alisema yuko tayari kukabiliana na wawaniaji wengine kwa wadhifa huo ambao wanapendekezwa na mbunge wa Kapseret Oscar Sudi.

• Sudi alikosoa uamuzi wa Mandago kugombea kiti cha Seneti akimtaka awachie wagombeaji wengine kuwania kiti hicho.

• Sudi aliwatambulisha wawaniaji wawili ambao watapambana katika kutafuta kiti cha useneta wa kaunti hiyo.

mandago-jackson
mandago-jackson

Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago amesisitiza kwamba atawania kiti cha useneta.

Mandago siku ya Jumanne alisema yuko tayari kukabiliana na wawaniaji wengine kwa wadhifa huo ambao wanapendekezwa na mbunge wa Kapseret Oscar Sudi.

Sudi alikosoa uamuzi wa Mandago kugombea kiti cha Seneti akimtaka awachie wagombeaji wengine kuwania kiti hicho.

Mandago amehudumu kama gavana wa Uasin Gishu kwa mihula miwili na kulingana na sheria haruhusiwi tena kuania wadhifa huo kwa muhula wa tatu, hali ambayo imemlazimu kutangaza kuania useneta ili kusalia katika ulingo wa siasa.

Mandago alisema ana haki kisheria kuwania kiti hicho akiungwa mkono na wananchi.

Sudi aliwatambulisha wawaniaji wawili ambao watapambana katika kutafuta kiti cha useneta wa kaunti hiyo.

Alimsihi gavana Mandago kuachana na wadhifa wa useneta na badala yake aende atafute nafasi katika ulingo wa kitaifa.