Uhuru, Ruto waongoza Wakenya kumuomboleza Dkt Richard Leakey

Muhtasari

•Dkt Richard Leakey aliyeaga dunia siku ya Jumapili akiwa na umri wa miaka 77

Dkt Richard Leakey
Dkt Richard Leakey
Image: Hisani

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta wamemuomboleza aliyekuwa mkuu wa wa utumishi wa Umma, Dkt Richard Leakey ambaye aliaga  dunia siku ya Jumapili akiwa na umri wa miaka 77 

Rais alimtaja Leakey kama mtetezi na mwazilishi wa tasisi mingi humu nchini.

"Dkt Leakey atakumbukwa kwake katika masuala ya uanaharakati na alifanikiwa kuanzisha taasisi kadhaa, likiwemo shirika lla wildlifeDirect" Rais Uhuru alisema

Leakey ambaye alikuwa mwandani wa Charles NJonjo alifariki muda mfupi baada ya kifo cha  Njonjo kutangazwa.

Naibu wa Rais, William Ruto kupitia ukurasa wake wa Twitter alimtaja Leakey kama mwenye kipawa na  bidii katika kazi zote za serikali ambazo alikabidhiwa kutekeleza.  

"Dkt Leakey alikuwa mwanapalaeoanthropolojia na Mhifadhi mwenye kipawa, mwenye bidii na aliyedhamiria ambaye alitekeleza ahadi zake kwa bidii." Ruto alinakiri kwa mtandao 

Aliendelea kumtaja Leakey kama shujaa aliyepigania nchi, kupitia juhudi zake  katika uhifadhi na utumishi wa umma. 

"Alipigania kishujaa nchi iliyo bora kupitia juhudi zake katika uhifadhi, siasa na utumishi wa umma, mara nyingi akifanya vyema katika nyanja tofauti na kuwatia moyo Wakenya wengi kwa uaminifu wake kwa nchi yake. Aliipenda Kenya. Pumzika kwa Amani Dr Richard Leakey" 

Dkt Leakey aliwahi kuhudumu kama mkurugenzi wa Makavazi ya kitaifa na mwenyekiti wa  bodi ya shirika la KWS