Mzee aliyetekwa nyara Murang'a afariki akiwa na umri wa miaka 103

Muhtasari
  • Mwaga aligonga vichwa vya habari alipotekwa nyara na wanaume wawili waliokuwa wakitaka kumpora vitu vyake
Mzee aliyetekwa nyara Murang'a afariki akiwa na umri wa miaka 103
Image: Alice Waithera

Mzee mmoja aliyetekwa nyara mwaka jana katika kaunti ya Murang'a amefariki.

Thomas Mwaga, 103, alifariki wikendi katika kaunti ya Murang'a.

Mwaga aligonga vichwa vya habari alipotekwa nyara na wanaume wawili waliokuwa wakitaka kumpora vitu vyake.

Wanaume hao wawili walimdanganya kwamba kulikuwa na dili ambayo ingemfanya apate Sh200,000.

Lakini alitilia shaka na kujaribu kutoroka kabla hawajamlazimisha kuingia kwenye gari.

Wanaume hao wawili walijua kuwa Mwaga alikuwa kwenye Sacco na wakajaribu kumlazimisha atoe pesa hizo katika tawi la Maragua.

Lakini wakiwa njiani, Mwaga alianza kuwasalimia wakazi na hata kuwatambua wengine.

Hili lilifanya wanaume hao waogope na kumrudisha kwenye gari kabla hawajaondoka kwa kasi.

Baadaye washukiwa hao walikamatwa na kufikishwa mahakamani.