Bei ya mbolea kuongezeka hadi 7,000 kufuatia vita Ukraine

Muhtasari

• Bei ya mbolea inatarajia kupanda hadi shilingi 7,000 kwa mfuko wa kilo 50 kutokana na vita vinavyoendelea katiya  urusi na Ukraine.

• Kulingana na waziri wa kilimo Peter Munya, Kenya inaagiza mbolea kutoka taifa la Urusi na China ,huku  vurumai zinazoendelea Ukraine zikikisiwa kuathiri usambazaji wa mbolea duniani.

KWA HISANI
KWA HISANI
Image: Africanbusinesscomm.com

Bei ya mbolea inatarajia kupanda hadi shilingi 7,000 kwa mfuko wa kilo 50 kutokana na vita vinavyoendelea katiya  urusi na Ukraine.

Kulingana na waziri wa kilimo Peter Munya, Kenya inaagiza mbolea kutoka taifa la Urusi na China ,huku  vurumai zinazoendelea Ukraine zikikisiwa kuathiri usambazaji wa mbolea duniani.

“Tunapata asilimia kubwa ya mbolea kutoka Urusi, na kufuatia vita vinavyoendelea katika taifa hilo, huenda bei ya mbolea ikafika shilingi 7,000 iwapo hatutapata njia mbadala,” Munya alisema.

Hatua hii inajiri huku wakulima wakiendelea kulalamikia bei ghali ya mbolea kwa sasa ambayo ni shilingi 6,000 kwa kile kinachotajwa kuwa kuongezeka kwa bei za gesi katika mataifa ya Yuropa.

Kulingana na Munya, serikali kuu inahitaji shilingi bilioni 31.8 ili kutafuta mbolea mbadala kwa wananchi ambapo wakulima watanunu mfuko wa kilo 50 kwa shilingi 2,800.

Kamati ya bunge inayojihusisha na kilimo ilimtaka waziri Munya kupendekeza bajeti ambayo inaweza kufanikisha mchakato wa kupunguza bei za mbolea.