Mbunge Rigathi Gachagua agura Jubilee, ajiunga na UDA

Muhtasari
  • Alisema hatajiunga na Muungano wa Azimio lakini ataambatana na chama cha Naibu Rais William Ruto
Mbunge wa Mathira Nderitu Gachagua
Mbunge wa Mathira Nderitu Gachagua

Nimekihama chama changu cha zamani JUbilee na kujiunga na UDA haya ni matamshi yake mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua baada ya kugura chama cha Jubilee.

Mbunge huyo pia alitoa wito kwa washindani wake kujiunga na chama kabla ya tarehe ya mwisho ya Ijumaa ili waweze kupata nafasi ya kukabiliana naye katika uteuzi wa chama.

Alisema hatajiunga na Muungano wa Azimio lakini ataambatana na chama cha Naibu Rais William Ruto.

Haya yanajiri siku moja baada ya mbunge wa Nandi Hills Alfred Keter kujiunga na chama hicho ambapo alikaribishwa na Gachagua.

"Nimekihama rasmi chama changu cha zamani cha Jubilee na kujiunga na Chama cha UDA siku zijazo

Nimelipa ada rasmi ya kutetea kiti cha Ubunge wa Mathira kwa tiketi ya UDA. Ninawaalika wale wote wanaotaka kunivua uanachama wa UDA kabla ya tarehe ya mwisho ya kesho na kunikabili katika uteuzi wa Chama kwa vile hawana nafasi ya kuwa katika Chama chochote kinachohusiana na Azimio," Aliandika Gachagua.

Gachagua amekuwa mkosoaji wa Rais Uhuru Kenyatta katika siku za hivi majuzi.

Mnamo Jumatatu, alitangaza hadharani kwamba hendisheki baina ya Uhuru na Raila hakukusudiwa Wakenya bali kulinda familia ya Kenyatta na biashara.