Mhudumu wa bodaboda amnyonga mwenzake Syokimau

Polisi walisema mshukiwa alimnyonga Otiende kwa mikono yake.

Muhtasari

• Kamanda wa polisi wa Machakos Issa Mohamed alisema wanamsaka mshukiwa ambaye tayari ametambulika. 

 

Maktaba
Maktaba

Mwanamume mmoja amekwenda mafichoni baada ya kumnyonga mwenzake baada ya kupigana nje ya baa moja eneo la Syokimau, kaunti ya Machakos. 

Polisi walisema wanamsaka mhudumu wa bodaboda aliyetambulika kama Peter kuhusiana na kifo cha George Otiende, 35. 

Wawili hao walikuwa wamepigana nje ya baa moja kabla ya Peter kuokota chupa ya bia na kumpiga Otiende kichwani. Polisi walisema mshukiwa alimnyonga Otiende kwa mikono yake. Otiende alifariki papo hapo. 

Mshukiwa alichukuwa pikipiki yake na kutoroka. Polisi walisema hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho. 

Kamanda wa polisi wa Machakos Issa Mohamed alisema wanamsaka mshukiwa ambaye tayari ametambulika. 

Alisema bado hawajabaini kilichochochea mzozo kati ya wawili hao.  Mohamed alisema wawili hao walikuwa wanajuana na wanaonekana kutofautiana kwa sababu zisizojulikana.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia mati.