Tutafanya maandamano mengine Jumatano-Azimio yatangaza

Vilevile alizindua ukusanyaji wa saini ili kuishinikiza serikali ya rais William Ruto kuondoka madarakani

Muhtasari
  • Kiongozi huyo wa upinzani alitoa agizo hilo dakika chache baada ya kuongoza mkutano wa Azimio la Umoja Saba Saba katika Viwanja vya Kamukunji.
Waandamani wakati wa maandamano ya saba saba.
Waandamani wakati wa maandamano ya saba saba.
Image: DANIEL OGENDO

Muungano wa Azimio La Umoja One Kenya Alliance utafanya maandamano mengine nchini kote siku ya Jumatano.

Katika kikao na wanahabari kilichosomwa na kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Opiyo Wandayi, ambacho kilihudhuriwa na kinara wa ODM Raila Odinga, alisema hawatakoma hadi wasikizwe.

"Tumewaarifu (polisi) kwamba Jumatano ijayo nchi nzima itasimama huku Wakenya wa tabaka mbalimbali wakishiriki maandamano makubwa katika kila upana na upana wa nchi," alisema.

Viongozi hao wa Azimio walizungumza katika Wakfu wa Jaramogi Oginga Odinga ambapo walihutubia wanahabari baada ya kukamilika kwa maandamano ya Saba Saba.

Raila Odinga, mnamo Ijumaa, Julai 7, aliamuru wafuasi wake kuandamana hadi Central Park, Nairobi, kwa mkutano mwingine, licha ya polisi kumuonya dhidi ya kuongoza maandamano katika Wilaya ya Biashara ya Kati (CBD).

Kiongozi huyo wa upinzani alitoa agizo hilo dakika chache baada ya kuongoza mkutano wa Azimio la Umoja Saba Saba katika Viwanja vya Kamukunji.

Vilevile alizindua ukusanyaji wa saini ili kuishinikiza serikali ya rais William Ruto kuondoka madarakani